Na.Alex Sonna-DODOMA
AFISA Mwanadamizi Ofisi ya Rais Ikulu, Dk Fabian Madele,amerejesha fomu ya kuomba ridhaa ya kugombea Jimbo la Dodoma Mjini.
Dkt.Madele amerejesha fomu hiyo kwa Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Wilaya ya Dodoma Mjini Bi.Sophia Kibaba,mapema leo Julai 1,2025.
Zoezi la uchukuaji fomu katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) linaendelea nchi nzima ambapo watia nia tofauti wameendelea kujitokeza kwa ajili ya kuchukua fomu za Ubunge na Udiwani.