Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango ameshiriki Mkutano wa pembezoni wa Nchi Zinazoendelea (LDCs) ulioongozwa na Waziri Mkuu wa Nepal Mhe. Kadga Sharma Oil na kuhudhuriwa na mataifa rafiki yaliyoendelea. Mkutano huo umejadili tathimini ya utekelezaji wa azimio la Mkutano wa Tano wa Umoja wa Mataifa wa Nchi Zinazoendelea uliofanyika Doha nchini Qatar mwaka 2023.