Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango akiwasili katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) leo tarehe 09 Julai 2025 wakati akielekea Mkoani Arusha kwa ajili ya kufungua Kongamano la Kimataifa la Watunga Sera wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii Bara la Afrika litakalofanyika tarehe 10 Julai 2025.