Dodoma
Wakala ya Barabara za Vijijini na Mijini (TARURA) imetoa mafunzo elekezi ya kuwajengea uwezo watumishi wapya 98 wa kada ya Uhandisi,Fundi Sanifu, Maofisa Hesabu, Wachumi pamoja na Ununuzi na Ugavi.
Mafunzo hayo yamefanyika katika ukumbi wa Jiji-Mtumba katika Mji wa Serikali jijini Dodoma.
Mafunzo hayo yaliongozwa na Mkurugenzi wa Huduma Saidizi Bi. Azimina Mbilinyi akishirikiana na Idara nyingine TARURA Makao Makuu.
Pamoja na hayo watumishi hao wapya walitakiwa kufanya kazi kwa weledi na ufanisi na kufuata maadili ya utumishi wa umma wanapotekeleza majukumu yao ya kila siku.
Katika mafunzo hayo watumishi hao walipatiwa mada nyingine kuhusiana na sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma pia walikula viapo vya uadilifu wa utumishi wa umma kutoka Ofisi ya Rais,Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora.