Happy Lazaro, Arusha
Arusha .MJUMBE wa INEC Dkt Zakia Mohamed Abubakar amewataka amewataka waratibu na wasimamizi hao kuajiri watendaji wenye weledi katika vituo vya kupigia kura na kuvipa taarifa mapema vyama vya siasa wakati wa mchakato wa kuapisha mawakala.
Ameyasema hayo leo jijini Arusha wakati akifunga mafunzo hayo kwa waratibu wa uchaguzi ,na wasimamizi wa uchaguzi ,na wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya jimbo yaliyofanyika kwa muda wa siku tatu yakiwa na lengo la kukumbushana majukumu ya Tume katika uratibu usimamizi na uendeshaji wa uchaguzi .
Amesema kuwa ,katika mafunzo hayo wamepitishwa katika maeneo mbalimbali ambayo sio mageni kwao .
Dkt. Zakia amesema kuwa maeneo mapya anaamini wameyaelewa hususani namna ya kushughulikia maombi ya watu wanaoomba kupiga kura.
Amesema kuwa ,wana jukumu kubwa la kutoa mafunzo kwa wasimamizi wasaidizi wa uchaguzi ngazi ya kata mafunzo watakayowapa yatawawezesha kuratibu na kusimamia uchaguzi ngazi ya kata vizuri na kwa weledi.
” jukumu lenu ni kutoa mafunzo sahihi kwa kuonyesha kwa vitendo yote wanayotakiwa kuyafanya wasimamizi wasaidizi ngazi ya kata sambamba na kuyatafasiri mafunzo hayo kwenye usimamizi wao wa shughuli za kila.siku za maswala ya uchaguzi kwa kuanza na vikao na vyama vya siasa .”amesema Dkt Zakia .
Kwa upande wa Mwenyekiti wa mafunzo hayo ,Shaban Ferdinand Manyama amesema kuwa, washiriki hao ni kutoka mikoa ya Arusha na Manyara ambapo washiriki walikuwa 86 ambao kimsingi tangu wameingia wote wameweza kushiriki na wameweza kupata mafunzo kuhusu mada ya uteuzi ,taratibu za kuwapata wagombea wanaotakiwa pamoja na watu wanaotakiwa kuweka pingamizi na namna ya kushughulikia rufaa pmoja na swala la maadili na uchuguzi kwa ujumla wake .
Amesema kuwa ,waliweza kupitishwa pia kwenye swala la kituo cha kupigia kura na kuhesabia kura watendaji wanaotakiwa kuwepo katika vituo vya kupigia kura na kuhesabia kura taratibu za kuhesabu kura na kutoa matokeo ya uchaguzi ,na wamefundishwa pia namna ya mapokezi ya vifaa pamoja na utunzaji wa vifaa na ukusanyaji wa vifaa vya uchaguzi matumizi ya fedha za uchuguzi ambao kwa msisitizo mkubwa wanaelekezwa fedha hizo zitumike kwa mustakabali wa matumizi ya uchaguzi na sio vinginevyo.
“Pia tumepitishwa kwenye upigaji wa kura ya Rais katika kituo tofauti na kituo ambacho mpiga kura amejiandikisha na Sheria ya gharama za uchaguzi”amesema Manyama