Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (wa pili kushoto), akiimba wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki, wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Dharura wa Baraza la Kisekta la Mawaziri Wanaosimamia Masuala ya Fedha na Uchumi (SCFEA) wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), uliofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, jijini Arusha. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe (wa pili kulia), Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki), Mhe. Dennis Londo (wa kwanza kushoto) na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban (kulia).
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb), akizungumza jambo wakati wa Mkutano wa Kwanza wa Dharura wa Baraza la Kisekta la Mawaziri Wanaosimamia Masuala ya Fedha na Uchumi (SCFEA) wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), uliofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, jijini Arusha, ambapo pamoja na mambo mengine ulijadili hatua za kikodi zilizo kwenye sheria za fedha za nchi wanachama zenye kuleta athari za kubagua bidhaa zilizozalishwa ndani ya nchi za Jumuiya.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (Katikati), Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe (kulia) na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki), Mhe. Dennis Londo (kushoto), wakiteta jambo kabla ya kuanza kwa Mkutano wa Kwanza wa Dharura wa Baraza la Kisekta la Mawaziri Wanaosimamia Masuala ya Fedha na Uchumi (SCFEA) wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), uliofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, jijini Arusha.
Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba Madelu (Mb) (kushoto), akiteta jambo na Mkurugenzi wa Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Prof. Claver Lumana Pashi (kulia), baada ya kutamatika kwa Mkutano wa Kwanza wa Dharura wa Baraza la Kisekta la Mawaziri Wanaosimamia Masuala ya Fedha na Uchumi (SCFEA) wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), uliofanyika Makao Makuu ya Jumuiya hiyo, jijini Arusha. Katikati ni Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe.(Picha na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini, WF, Arusha)
…….
Na Benny Mwaipaja, Arusha
Baraza la Kisekta la Mawaziri Wanaosimamia Masuala ya Fedha na Uchumi (SCFEA) wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), wamekubaliana kuandaa orodha ya bidhaa zitakazohusika na uondoaji wa kodi na ushuru mbalimbali ikiwa ni utekelezaji wa itifaki ya ushirikiano ili kuchochea biashara na uwekezaji katika Jumuiya hiyo.
Makubaliano hayo yameelezwa na Waziri wa Fedha, Mhe. Dkt. Mwigulu Lameck Nchemba (Mb), ambaye ameongoza Ujumbe wa Tanzania katika Mkutano wa Kwanza wa Dharura wa Baraza la Kisekta la Mawaziri Wanaosimamia Masuala ya Fedha na Uchumi (SCFEA) wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) uliofanyika Makuu ya Jumuiya hiyo, jijini Arusha.
Hatua hiyo ni utekelezaji wa maelekezo ya Mkutano wa 46 wa Baraza la Kisekta la Mawaziri wa Biashara, Viwanda, Fedha na Uwekezaji (SCTIFI) na makubaliano ya Mawaziri wa Fedha wakati wa mashauriano ya kibajeti katika mikutano yao iliyofanyika mwezi Mei 2025.
Mhe. Dkt. Nchemba amesema kuwa Mkutano huo umejadili pamoja na mambo mengine, hatua za kikodi zilizo kwenye sheria za fedha za nchi wanachama zenye kuleta athari za kubagua bidhaa zilizozalishwa ndani ya nchi za Jumuiya.
Mkutano huo umehudhuriwa na wajumbe kutoka Tanzania Bara na Zanzibar, wakiwemo, Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara, Mhe. Exaud Kigahe, Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki (anayeshughulikia masuala ya Afrika Mashariki), Mhe. Dennis Londo, Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Fedha, Bi. Amina Khamis Shaaban.