Mkurugenzi Mkuu- Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead Teri akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 25, 2025 skuelekea uzinduzi wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji cha Kisasa (EACLC), takayofanyika Agosti 2, 2025, katika eneo la mradi lililopo Ubungo jijini Dar es Salaam.
Katibu kutoka Idara ya Uratibu na Ufatiliaji Wilaya ya Ubungo, Andambike Kyomo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 25, 2025 skuelekea uzinduzi wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji cha Kisasa (EACLC), takayofanyika Agosti 2, 2025, katika eneo la mradi lililopo Ubungo jijini Dar es Salaam.
Mratibu kutoka Kituo cha Biashara na Usafirishaji cha Kisasa (EACLC), Cathy Wang Katibu kutoka Idara ya Uratibu na Ufatiliaji Wilaya ya Ubungo, Andambike Kyomo akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam leo Julai 25, 2025 skuelekea uzinduzi wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji cha Kisasa (EACLC), takayofanyika Agosti 2, 2025, katika eneo la mradi lililopo Ubungo jijini Dar es Salaam.
RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt.Samia Suluhu Hassan, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Biashara na Usafirishaji cha Kisasa (EACLC), takayofanyika Agosti 2, 2025, katika eneo la mradi lililopo Ubungo jijini Dar es Salaam.
Hii ni hafla ya kihistoria itakayozindua rasmi kituo kikubwa na cha kisasa zaidi cha biashara na usafirishaji nchini, ambacho kinatarajiwa kuwa kitovu cha shughuli za kiuchumi, biashara na uwekezaji si tu kwa Jiji la Dar es Salaam bali pia kwa ukanda mzima wa Afrika Mashariki.
Akizungumza na waandishi wa habari leo Julai 25, 2025, Mkurugenzi Mkuu- Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead Teri amesema kuwa mradi huo wa kimkakati umetekelezwa kwa ushirikiano kati ya Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalum ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), East Africa Commercial & Logistics Center Limited (EACLC), na Halmashauri ya Manispaa ya Ubungo, kwa lengo la kuboresha mazingira ya biashara na kuongeza ufanisi katika sekta ya usafirishaji na biashara ya jumla nchini.
Teri ameeleza kuwa mradi huo umegharimu zaidi ya Dola za Marekani milioni 110 (sawa na Shilingi bilioni 282.7 za Kitanzania) na unajumuisha jumla ya sehemu 2,060 za maduka na ofisi. Aidha, unatarajiwa kuleta ajira zaidi ya 15,000 za moja kwa moja, pamoja na ajira zisizo rasmi zipatazo 50,000, hivyo kuwa kichocheo muhimu cha ukuaji wa uchumi wa Taifa.
“Uzinduzi wa kituo hiki ni kielelezo cha utekelezaji wa maono na dhamira ya Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kujenga uchumi jumuishi, wa viwanda na wenye ushindani katika soko la kikanda na kimataifa,” amesema Teri.
Akijibu maswali ya waandishi wa Habari teri amewaondoa wasiwasi wafanyabiashara wa Kariakoo kuwa halitaenda kubadilisha soko la kariakoo bali litaenda kusaidia kwani nafasi kubwa zaidi itajitokeza pamoja na kupanua ukubwa wa biashara na shughuli za kiuchumi.
Kwa kuzingatia umuhimu wa tukio hilo, TISEZA inatoa wito kwa wananchi, wawekezaji wa ndani na nje ya nchi, taasisi za kifedha, mashirika ya umma na binafsi, wafanyabiashara, wajasiriamali, na wadau wote wa maendeleo kuhudhuria kwa wingi katika hafla hii na kutumia kikamilifu fursa mbalimbali za kiuchumi na uwekezaji zitakazopatikana kupitia kituo hiki cha kisasa.

Mkurugenzi Mkuu Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA), Gilead Teri akipewa maelezo na Cathy Wang alipotembelea Kituo cha Biashara na Usafirishaji cha Kisasa (EACLC), takayofanyika Agosti 2, 2025, katika eneo la mradi lililopo Ubungo jijini Dar es Salaam.