MIAMI: NYOTA wa soka, Lionel Messi na mkewe Antonela Roccuzzo walionekana wakifurahia tamasha la Coldplay Miami, siku chache baada ya kashfa ya busu lililowahusisha Mkurugenzi Mkuu Mtendaji wa Mwanaastronomia Andy Byron na Mkuu wa HR Kristin Cabot.
Picha ya mkurugenzi huyo na Mkuu wa HR ndiyo iliyokuwa ikitamba siku chache zilizopita kabla ya kuzimwa na picha ya Messi na Mkewe wakiwa mapumzikoni katika tamasha hilo la Coldplay na kuzua jumbe mbalimbali za mashabiki.
Nyota huyo na mkewe, Antonela Roccuzzo, walionekana wakifurahia tamasha la Coldplay kwenye Uwanja wa Hard Rock huko Miami, na mashabiki wao hawakuwa nyuma kuwafurahia.
Katika mtandao wa X wa tamasha hilo la Coldplay wamechapisha video ya mwanasoka huyo wa Argentina na mkewe wakiwa katika eneo hilo na furaha mno huku akiwapungia mkono watu katika ukumbi huo mkewe akiwa amesimama kando yake, pia akitabasamu na kufurahia muziki.
Uwepo wa Messi katika tamasha hilo umefanya tamasha hilo kuwa na hamasa kama mashindano ya Kombe la Dunia la FIFA.
Klipu hiyo fupi ilisambaa haraka, huku wengi wakiita wimbi la Messi ‘kama mfalme’ na kusifu uwepo wa watu hao wawili wenye mapenzi ya utulivu na neema
The post Busu la Mwanaastronomia, HR lazimwa na Messi, first appeared on SpotiLEO.