LOS ANGELES: MSANII nyota wa Bongo Fleva, Naseeb Abdul ‘Diamond Platnumz’, ameendelea kuthibitisha kuwa si tu staa wa muziki bali pia ni mfalme wa maisha ya kifahari, baada ya kuonesha mjengo wa kifahari aliofikia huko Los Angeles, Marekani.
Kupitia mitandao yake ya kijamii, Diamond ameposti video na picha akiingia kwenye jumba hilo pamoja na timu yake, ambalo wamepanga kulikaa kwa muda wakati wa shughuli zao za kikazi na mapumziko.
Staa huyo wa amesema kuwa anaamini katika kuishi maisha mazuri, na kwamba si jambo la kujisifu bali ni sehemu ya matokeo ya juhudi zake za miaka mingi kwenye muziki.
“Napenda kuishi maisha mazuri… na ninayamudu. Si tu kwa sababu ya pesa, bali kwa sababu najituma na najua thamani ya kazi yangu,” alisema Diamond.
Mashabiki wake wameendelea kumpongeza kwa mafanikio hayo huku wengine wakieleza kuwa ni motisha kwa wasanii wengine wa Afrika kuamini ndoto zao na kufanya kazi kwa bidii.
Diamond na timu yake wamekuwa Marekani kwa shughuli mbalimbali ikiwemo kurekodi muziki mpya, mikutano ya kimataifa ya biashara ya burudani, na mapumziko mafupi.
The post Diamond aonesha mjengo wa kifahari na ujumbe mzito first appeared on SpotiLEO.