Β
ππ π πππππ: Klabu ya Simba Sc imethibitisha kumsajili kiungo mshambuliaji, Morice Abraham (21) raia wa Tanzania kwa mkataba wa miaka miwili akitokea klabu ya Spartak Subotica ya Serbia.
Simba Sc imeeleza kuwa baada ya kurejea nchini kutoka Serbia nyota huyo wa timu ya taifa ya Tanzania alifanya mazoezi na Wekundu hao wa Msimbazi ambapo kocha Fadlu Davids na wasaidizi wake walimpitisha hivyo uongozi ukamsajili moja kwa moja.
Morice ambaye amekulia katika Kituo cha kukuzia vipaji cha Alliance Academy cha jijini Mwanza anakumbukwa kuwa na nahodha wa timu ya vijana ya Tanzania chini ya umri wa miaka 17 βSerengeti Boysβ kilichoshiriki AFCON mwaka 2019 ambayo Tanzania alikuwa mwenyeji.
Msimu uliopita akiwa katika klabu yake ya Spartak Subotica, Morice alifunga mabao mawili na kusaidia βassistsβ mengine manne.
Morice atajiunga na kikosi kilichopo kambini nchini Misri muda wowote kutoka sasa mara baada ya kukamilika kwa vibali vyake vya kusafiria.
βΒ