Mshambuliaji wa Slovenia kutoka RB Leipzig, Benjamin Sesko (22), anatumia mbinu za kisiasa katika usajili kwa kuzitumia Newcastle na Manchester United kuzipambanisha ili apate dili bora zaidi.
Newcastle wameonyesha nia mpya ya kumsajili beki wa kati wa England, Marc Guehi, kwa ofa ya takriban pauni milioni 40, lakini Crystal Palace wanataka pauni milioni 50 ili kumuachia mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25.
Kocha David Moyes anataka kufanya usajili wa hadi wachezaji sita zaidi kwa ajili ya Everton, ikiwa ni pamoja na viungo wa kati wawili na wachezaji wa pembeni wawili.
Tottenham wameambiwa watalazimika kulipa euro milioni 30 (pauni milioni 26) ili kumsajili kiungo wa Hispania Marc Casado (21) kutoka Barcelona.
Winga wa Brazil Rodrygo (24) anataka kubaki Real Madrid licha ya kuvutiwa na Tottenham, Arsenal na Liverpool.
Crystal Palace wanakabiliana na ushindani kutoka Juventus katika harakati za kumsajili beki wa kulia wa Girona, Arnau Martinez (22) raia wa Hispania.
Kiungo wa kati wa Napoli na Sweden, Jens Cajuste (25), anapendelea kurejea Ipswich Town kuliko kwenda Burnley au ligi ya Saudi Arabia.
Stuttgart wanakaribia kufanikisha dili la kumsajili kiungo wa kati wa Ureno, Fabio Vieira (25), kutoka Arsenal.
Porto walivutiwa na beki wa Poland Jakub Kiwior (25), lakini walikataa kutimiza thamani ya euro milioni 30 (pauni milioni 26) iliyowekwa na Arsenal.
Tottenham wanatataka kumuuza kiungo wa kati kutoka Mali, Yves Bissouma (28), ili kutoa nafasi kwa Conor Gallagher, kiungo wa kati wa England mwenye umri wa miaka 25 kutoka Atletico Madrid.
Liverpool wanafuatilia maendeleo ya beki wa Brentford na timu ya taifa ya Ireland, Nathan Collins (24).
West Ham wamewasilisha ofa mpya ya pauni milioni 10 kwa Botafogo ili kumsajili kipa wa Kibrazil John Victor (29).
Bayer Leverkusen wanamtaka mshambuliaji wa Denmark wa Manchester United, Rasmus Hojlund (22), lakini wanakumbana na ushindani kutoka AC Milan, Inter Milan na Juventus.