Shirikisho la Soka Afrika (CAF) Laipiga Faini TFF Dola 10,000 Kisa Hichi
Shirikisho la Soka Afrika (CAF) limeitoza Shirikisho la Soka Tanzania TFF, faini ya Dola 10,000 (takriban Tsh. Milioni 25) kwa kuvunja masharti ya usalama na ulinzi yaliyoainishwa katika lbara ya 82 na 83 za Kanuni za Nidhamu za CAF pamoja na lbara ya 24 na 28 za Kanuni za Usalama na Ulinzi.
Adhabu huyo iliyotolewa na Bodi ya Nidhamu ya CAF imetokana na tukio la ukiukwaji wa taratibu za usalama wakati wa mechi kati ya Tanzania dhidi ya BurkinaFaso kwenye Michuano ya CHAN 2024 inayoendelea ambapo mashabiki walifanya vitendo vya utovu wa nidhamu katika mchezo huo uliomalizika kwa Tanzania kushinda Magoli 2-0.
Aidha Bodi hiyo imeipiga faini Shirikisho la Soka Kenya (FKF) Dola 5,000 (takriban Tsh. Milioni 12) kwa sababu ya msongamano wa watu (stampede) na kuingia bila idhini na Dola 10,000 (takritban Tsh. Milioni 25) kwa kosa la kuwashambulia Wafanyakazi wa CAF na wageni