DAR ES SALAAM: TIMU ya Taifa Stars inaendelea kuvuna ilichokipanda, hii inakuja baada ya kupokea zawadi za pongezi kwenye kila mchezo wanaoshida.
Ifahamike kwamba Rais, Samia Suluhu Hassan aliwapa ahadi vijana wa timu hiyo kuwa ikiwa watashinda ubingwa wa CHAN basi atawapa zawadi ya shilingi bilioni moja kama haitoshi Rais pia aliahidi kulinunua kila bao watakalofunga Stars kwenye michuano ya CHAN kwa shilingi Sh milioni 10.
Baada ya ahadi za Rais Samia wadau mbalimbali nao wamekuwa wakimuunga mkono.
Kwenye mchezo dhidi ya Burknafaso Stars ilishinda 2-0 hivyo ilivuna milioni 20 za goli la Mama, Waziri wa Habari, Utamaduni Sanaa na Michezo, Prof Palamagamba Kabudi pia aliwapatia Sh milioni 20 lakini pia Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Albert Chalamila aliwazawadia milioni 20 jumla ikawa milioni 60.
Mchezo wa pili Taifa Stars ilishinda 1-0 dhidi ya Mauritania ambapo walivuna milioni 10 ya goli la Mama wakalamba milioni 20 ya Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam na mfanyabiashara Azim Dewji akawapatia milioni 25 na kufanya jumla kuwa milioni 55.
Mchezo wa jana walivuna Sh milioni 20 za goli Mama wakapata milioni 20 za Mkuu wa Mkoa wa Dar Es Salaam na wakapata pia Sh milioni 20 za Wizara ya michezo na kisha wakapokea Sh milioni 25 kutoka kwa wafanyabishara na kufanya kuwa jumla ya Sh milioni 85 lakini Msemaji Mkuu wa Serikali, Gerson Msigwa aliahidi kufanya maarifa zifikie Sh milioni 100.
Hivyo kwenye michezo mitatu Taifa Stars iliyocheza hadi sasa imevuna jumla za Sh milioni 215 kama zawadi ya ushindi, ikumbukwe kuwa tayari imejihakikishia pia nafasi ya robo fainali ya michuano hiyo na ikiwa watatinga nusu fainali watapewa Sh milioni 200 ambayo pia ni ahadi ya Rais Samia.
The post Taifa Stars kibosi tu CHAN first appeared on SpotiLEO.