RIYADH: MPENZI wa mwanasoka Cristiano Ronaldo, Georgina Rodriguez amethibitisha kuchumbiwa na mwanasoka huyo baada ya kuweka picha ya pete yake ya uchumba kwenye ukurasa wake wa Instagram huku mkono wake ukiwa juu ya mkono wa Ronaldo.
Mpenzi huyo wa Ronaldo mwenye miaka 40, Georgina anamiaka 31 na katika chapisho hilo ameandika: “Ndiyo ninakubali. Katika hili na maisha yangu yote.”
Wapenzi hao wamekuwa pamoja tangu 2016 na mwanamitindo huyo hapo awali alizua tetesi za uchumba mapema mwaka huu baada ya kuweka picha ya pete tofauti tofauti kidoleni mwake.
Wakati huo huo, Ronaldo alikuwa amemtaja Georgina kama mke wake walipohudhuria Tuzo za Globe Soccer pamoja huko Dubai mwaka jana.
Ronaldo, ambaye ambaye ameongeza mkataba wa miaka miwili wa kuitumikia klabu ya Al-Nassr Fc ya Riyadh, Saudi Arabia hadi mwaka 2027, aliwahi kusema kuwa ana uhakika wa asilimia 1,000 kwamba yeye na Georgina watafunga ndoa.
Alisema: “Sikuzote mimi humwambia, kama kila kitu kwenye maisha yetu, naye anajua ninachozungumzia.
“Inaweza kuwa katika mwaka mmoja au inaweza kuwa katika miezi sita au inaweza kuwa katika mwezi. Nina uhakika wa asilimia 1,000 kuwa itafanyika.”
Georgina amefichua kuwa marafiki zake wamekuwa wakiuliza mara kwa mara ni lini yeye na Cristiano watafunga ndoa.
Alisema: “Sikuzote wao hutania kuhusu harusi. ‘Harusi itakuwa lini?’
“Tangu wimbo wa Jennifer Lopez ‘The Ring or When’ ulipotoka, walianza kuniimbia. Na vizuri, hii sio juu yangu.”
Rodriguez alikumbuka jinsi alivyokutana kwa mara ya kwanza na Cristiano Ronaldo alipokuwa akifanya kazi kwenye duka la Gucci huko Madrid.
Alisema: “Mwishowe niliweza kuondoka dukani na kurudi nyumbani saa tatu baadaye kuliko nilivyopaswa, na nilipokuwa nikijiandaa kuondoka Cristiano aliingia na motto wake mkubwa pamoja na marafiki zake kadhaa.
Ronaldo ambaye amewahi kucheza klabu kubwa ikiwemo Manchester United na Real Madrid ilikuwa vigumu kukubali jambo hilo lakini nafuraha kwani kwa sasa watoto wake nao wanaushindani mkubwa wanataka kuwa na mafanikio kama baba yao.
Akiongea kwenye podikasti ya Rio Ferdinand Presents, alisema: “Nilikuwa kwenye Bahari Nyekundu siku kadhaa zilizopita, nacheza padel kila siku. Mimi na Cristiano Jr. huwa tunakasirikiana, hatuongei kwa siku hadi mbili.
“Hii ndiyo sababu nina furaha, hata yule mdogo Mateo anapata ushindani, napenda. Inaonesha wanautu na tama ya mafanikio kama baba yao.
Nyota huyo wa Ureno kwa sasa ni baba wa Cristiano Jr mwenye miaka 15, na mapacha Eva Maria na Mateo, pamoja na binti Alana, saba, na Bella pamoja na Georgina.
The post Hatimaye Cristiano Ronaldo na Georgina wachumbiana first appeared on SpotiLEO.