Klabu ya kaskazini mwa London ya Tottenham sasa inahusishwa na mmoja wa washambuliaji chipukizi bora zaidi wa kiBrazil, Savinho wa Manchester City.
Kwa mujibu wa The Athletic, Spurs wamewasiliana na Man City kuhusu nia yao ya kumsajili mchezaji huyo na inaelezwa mazungumzo yamekuwa yakiendelea katika siku za karibuni.
Taarifa zinaweka wazi kuwa City wako tayari kumuuza Savinho ikiwa tu anataka kuhama, na ikiwa hali itakuwa hivyo basi watahitaji dau la pauni milioni 50 ili kumruhusu aondoke.