Wachezaji wa klabu ya Chelsea wameamua kutoa sehemu ya bonasi zao za ushindi wa Kombe la Dunia ngazi ya Klabu kwa familia za wachezaji Diogo Jota na André Silva waliofariki kwa ajali ya gari mwezi Julai 3,2025.
Chelsea walitwaa taji hilo julai 13 na kuvuna zaidi ya shilingi bilioni 302 za Kitanzania kama zawadi ya ushindi huku wachezaji wakitengewa bilioni 41 za Kitanzania kama bonasi.
Wachezaji hao ambao kila mmoja anakadiriwa kupata bonasi ya Bilioni 1 walikubaliana kutoa sehemu ya bonasi hiyo kwa familia ya Jota aliyekuwa nyota wa Liverpool na mdogo wake Andre Silva waliofariki kwa pamoja Nchini Hispania.