LONDON: MENEJA wa Chelsea Enzo Maresca amewaambia waandishi wa Habari kuelekea mechi yao ya ufunguzi wa Ligi kuwa anakuna Kichwa kuziba pengo katika safu ya ulinzi ya klabu hiyo baada ya beki wake wa kati Levi Colwill kupata jeraha la ACL.
Colwill alipata jeraha hilo akiwa mazoezini na amefanyiwa upasuaji uliofanikiwa, huku mchezaji huyo wa kimataifa wa Uingereza mwenye umri wa miaka 22 akitarajiwa kukosa sehemu kubwa ya msimu huu mpya.
Kwa kawaida huchukua muda wa angalau miezi sita hadi tisa kwa mchezaji kupona jeraha la ACL na kurejea uwanjani huku akiwaacha Chelsea bila mtu wa kutumainia katika safu yao ya ulinzi.
“Yuko sawa lakini anafahamu kwamba lazima awe nje kwa muda mrefu. Ni hasara kubwa kwetu. Alikuwa muhimu sana msimu uliopita. Tuna uwezo wa kutengeneza nafasi na kushambulia vizuri kama tunaweza kujenga shambulizi kuanzia nyuma. Levi alikuwa sehemu kubwa ya hilo Nadhani tunahitaji beki mpya wa kati.” – Maresca aliwaambia wanahabari.
Chelsea wanatazamia kuendeleza mafanikio ya msimu uliopita baada ya kumaliza katika nafasi ya nne za juu kwenye Ligi na kushinda Kombe la Dunia la klabu. Tayari wameingia sokoni na kuchukuwa wachezaji kadhaa kama Joao Pedro, Jamie Gittens, Jorrel Hato, Liam Delap, Estevao Willian, na wengineo. Huku wakiwafata Palace kwa tahadhari kwakuwa walishawaduwaza vigogo Manchester City na mabingwa Liverpool katika mechi zao za mwisho.
The post Maresca akuna Kichwa jeraha la Colwill first appeared on SpotiLEO.