KIGALI: MCHEZAJI wa Yanga SC, Pacome Zouzoua, ameonesha furaha yake baada ya kuanza kwa kishindo msimu mpya, kufuatia ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya Rayon Sports ya Rwanda katika mchezo wa kimataifa wa kirafiki uliopigwa Uwanja wa Amahoro, Kigali jana.
Kupitia ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Zouzoua aliandika ujumbe mzito wa hamasa akisema:
“Msimu mpya, sura mpya! Nimefurahi kuanza safari hii na wachezaji wenzangu wapya. Tutapambana pamoja, kusaidiana na kulenga mafanikio makubwa. Umoja ni nguvu, ndani na nje ya uwanja tutakuwa familia. Ni muda wa kazi, kujituma na ushindi.”
Nyota huyo raia wa Ivory Coast alijiunga na Yanga mwaka juzi akitokea ASEC Mimosas, na ameendelea kuwa miongoni mwa wachezaji muhimu katika safu ya ushambuliaji ya mabingwa hao wa Tanzania Bara.
Yanga ilialikwa nchini Rwanda kwa mchezo huo wa kimataifa ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya msimu ujao wa Ligi Kuu na michuano ya Kimataifa.
The post Pacome: Nimefurahi kuanza safari na Kombe first appeared on SpotiLEO.