DAR ES SALAAM: Azam FC imeongeza nguvu katika kikosi chake baada ya kutambulisha wachezaji watatu wapya ambao ni Issa Fofana wa Ivory Coast, Taieb Zitoun na Barakat Hmidi wote wa Tunisia.
Wachezaji hao waliwahi kutumikia Al Hilal ya Sudan, timu aliyokuwa akifundisha Kocha Frorent Ibenge aliyejiunga na Azam FC msimu huu.
Issa Fofana ni kipa mwenye umri wa miaka 21, alitokea Al Hilal ya Sudan na amewahi kuwakilisha timu ya taifa ya vijana ya Ivory coast.
Taieb Zitoun, mshambuliaji wa miaka 28 kutoka Tunisia, alijiunga akitokea Al Hilal ya Sudan. Zitoun anatarajiwa kuongeza nguvu katika safu ya ushambuliaji ya Azam FC.
Barakat Hmidi, kiungo mshambuliaji wa miaka 22 kutoka Tunisia, alijiunga akitokea Club Sportif Sfaxien. Hmidi anatarajiwa kuleta ubunifu na nguvu katika kiungo cha timu.
Wachezaji hawa wapya wanatarajiwa kuimarisha kikosi cha Azam FC na kushirikiana na wachezaji wengine katika kambi ya maandalizi nchini Rwanda, tayari kwa msimu mpya wa Ligi Kuu na mashindano ya kimataifa.
Ikiwa Rwanda Azam itachezwa mchezo wa kimataifa wa kirafiki dhidi ya APR ya nchini humo.
The post Wachezaji wapya Azam FC wanafahamiana na Ibenge first appeared on SpotiLEO.