Kikosi cha wachezaji pamoja na viongozi wa timu ya Taifa ya soka ya Morocco, inayofahamika kama ‘Simba wa Milima ya Atlas’, kimewasili Dar es Salaam kwa maandalizi ya mchezo wa robo fainali ya CHAN 2024 dhidi ya ‘Taifa Stars’ ya Tanzania.
Mabingwa hao wa CHAN mara mbili watakutana na Tanzania katika mchezo utakaofanyika Agosti 22 mwaka huu katika Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.
Mashindano hayo ya CHAN 2024 yameandaliwa kwa ushirikiano wa Tanzania, Kenya, na Uganda.