LIVERPOOL: IMETHIBITISHWA kuwa beki mpya wa mabingwa watetezi wa EPL Liverpool Jeremie Frimpong atakuwa nje ya uwanja kwa wiki kadhaa kutokana na jeraha la misuli ya paja alilopata katika ushindi wao wa 4-2 dhidi ya Bournemouth dimbani Anfield ijumaa iliyopita.
Beki huyo wa zamani wa Bayer Leverkusen, aliyeripotiwa kuchukua nafasi ya Trent Alexander-Arnold kwa pauni milioni 29.5, alifanyiwa mabadiliko baada ya kucheza kwa dakika 60 mechi yake ya kwanza ya ligi akiwa na Liverpool.
“Timu ya Madaktari ilikuwa sahihi kabisa kuhusu kuumia na kuniambia nimuondoe Jeremie kikosini kwa mechi hii hatakuwepo hadi mwisho wa kipindi cha mapumziko ya kimataifa (Septemba 10) na maamuzi hayo yalifanyika wakati wa mchezo ule”.
“Najua nilikosolewa sana kwa kumtoa, siyo? Haikuwa na uhusiano wowote na jinsi alivyocheza lakini tulihisi alikuwa na tatizo kwenye misuli yake ya paja na kwetu, lilikuwa jambo zuri kumtoa, vinginevyo angekuwa nje kwa muda mrefu zaidi. Tunatarajia kuwa naye baada ya mapumziko ya kimataifa.” Amesema Slot
Conor Bradley, ambaye ni chaguo jingine la Liverpool la beki wa kulia, amerejea mazoezini jana Alhamisi baada ya kuwa majeruhi mwa muda. Mechi ya Jumatatu katika uwanja wa St. James’ Park imetawaliwa na Sakata la Liverpool na Alexander Isak, huku Magpies wakiripotiwa kutaka ada ya uhamisho ya pauni milioni 150 kwa mchezaji huyo wa kimataifa wa Sweden mwenye umri wa miaka 25.
The post Frimpong Yamemkuta! first appeared on SpotiLEO.