Siku ya Simba ni nafasi kubwa ya kuwapa heshima watu waliofanya makubwa ndani ya Simba , tunatambua , tunakumbuka na tunathamini mchango wao , mwaka huu kwenye Simba Day tutawaalika wachezaji wetu wawili wa zamani ambao wamefanya makubwa ndani ya Simba yetu”
“Nahodha wetu wa zamani ambaye amedunu Simba kwa miaka 6 , ambaye ametupa makombe 4 na ametupeleka Robo Fainali mara 4 , kwa sasa amestaafu rasmi soka hivyo ni nafasi ya sisi kumpa shukran John Rapahael Bocco”
“Lakini siku hiyo hiyo tutaenda kumuaga nahodha wetu mwingine aliyeitumikia Simba kwa miaka 15 , ameondoka mwaka juzi lakini hatukupata nafasi ya kumuaga”
“Hii ni fursa ya kipekee kwetu kumuaga kipenzi chetu Jonas Mkude” Amesema Ahmed Ally.