KIKOSI cha Simba leo Agosti 28 kinatarajiwa kuwasili nchini kikitokea Misri ambapo kiliweka kambi ya maandalizi ya msimu mpya unaotarajiwa kuanza hivi karibuni 2025/2026, huku kukiwa na tetesi za Simba kuandika barua ya kuomba kuto kucheza mchezo wao dhidi ya Yanga.
Ikumbukwe ya kwamba tarehe 16 sept kutakuwa na mtanange wa Kariakoo Dabi itakayowakutanisha miamba miwili ya soka kutoka nchini Tanzania, Simba na Yanga ukiwa ni mchezo wa Ngao ya Jamii.
Ukiashiria ufunguzi wa Ligi Kuu bara ya NBC, Huku kukiwa na tetesi za Simba kuandika barua kwa TFF kuomba kuto kucheza mchezo huo hiyo ni kutokana na Simba kuwa na mchezo wa kimataifa dhidi ya Gaborone United.
Meneja habari na mawasiliano wa klabu ya Simba Ahmed Ally ameeleza ya kwamba mchezo wao dhidi ya Yanga upo pale pale na Mnyama hajaandika barua yoyote ya kuomba kutocheza mchezo huo.
“Watu wanatafuta kiki kutoka kwetu kwasababu sisi Simba ni tmu kubwa hivyo wanazungumzia timu kubwa ili wapate kiki, lakini sisi tupo tayari kwaajili ya mchezo huo na hatujaandika barua yoyote” Alisema Ahmed Ally.
Ikumbukwe ya kwamba tetesi hizo zilianza kusikika baada ya CAF kutangaza ratiba ya mchezo wasimba dhidi ya Gaborone mchezo kuchezwa kati ya tarehe 18-21 hivyo ingekuwa ngumu kwa Simba kucheza mchezo huo wa Gaborone kama imetoka kucheza mchezo na Yanga hata masaa 72 yanayofahamika na FIFA baada ya kucheza mchezo ndio timu icheze mchezo mwingine yakiwa hayajakamilika.
Lakini ratiba rasmi imetoka Simba atacheza mchezo wake wa kwanza kimataifa msimu huu dhidi ya Gaborone mnamo tarehe 19 September