Klabu ya JKT Tanzania imetangaza kuwapa mkono wa kwaheri nyota wake wawili ambao ni golikipa wa Timu ya Taifa ya Tanzania (Taifa Stars), Yakoub Suleiman na beki Wilson NANGU hivyo hawatakuwa sehemu ya kikosi hicho kuelekea msimu ujao wa 2025/26.
Nyota hao wawili ambao walikuwa mhimili imara kwa maafande hao msimu uliopita wanaripotiwa tayari wamekamilisha uhamisho wao wa kujiunga na timu namba 5 kwa ubora barani Afrika, Simba Sc ya Tanzania.