LONDON: WASHIKA mitutu wa jiji la London Arsenal wamesema mshambuliaji wao Kai Havertz amefanyiwa upasuaji mdogo wa goti usiku wa Alhamisi baada ya kuumia katika mchezo wa ufunguzi wa msimu dhidi ya Manchester United.
Arsenal haikusema ni lini hasa Havertz atarejea lakini imesema muda si mrefu ataanza programu maalumu ya ‘recovery and rehabilitation program’, huku kila mmoja akimuunga mkono Kai ili kuhakikisha anarejea katika utimamu kamili haraka iwezekanavyo.
Havertz alikosa miezi kadhaa msimu uliopita kutokana na jeraha la misuli ya paja lakini ripoti za vyombo vya habari vya England zilisema anatarajiwa kukosa wiki chache.
Arsenal ilimsajili Eberechi Eze kutoka Crystal Palace baada ya Havertz kupata jeraha hilo katika mchezo dhidi ya United waliopata ushindi wa bao 1-0.
The post Kai afanyiwa upasuaji wa goti first appeared on SpotiLEO.