MANCHESTER: Kiungo wa kati wa Manchester United Kobbie Mainoo ameingia katika mzozo na klabu hiyo baada ya kuomba kuondoka Old Trafford kwa mkopo na United kukataa ombi hilo, wakimwambia klabu hiyo inamthamini na inataka abaki aendelee kupigania nafasi yake kikosini.
Mazungumzo baina ya mchezaji huyo na klabu yanaendelea na inabakia kuonekana ikiwa kuna matunda ya mazungumzo zaidi kuhusu suala hilo kabla ya tarehe ya mwisho ya usajili siku ya Jumatatu.
Mainoo, mwenye umri wa miaka 20, alicheza dakika zote 90 katika kipigo chao cha mikwaju ya penalti ya Kombe la Carabao Jumatano dhidi ya Grimsby na kuonesha kiwango kilichowaridhisha mashabiki wengi wa United.
Hata hivyo, hakupata hata dakika moja katika mechi zote mbili za ufunguzi za Ligi Kuu za United na meneja Ruben Amorim amemuweka wazi kuwa anapigania nafasi na nahodha Bruno Fernandes.
Mchezaji huyo wa kimataifa wa England bado ana mkataba hadi 2027 lakini mazungumzo ya kuongeza muda yamekwama. Huku ikifahamika kuwa hataki kuondoka United moja kwa moja lakini ana wasiwasi kuhusu muda wa mechi atakaopata.
The post United yaweka ngumu kwa Mainoo first appeared on SpotiLEO.