Klabu ya Manchester United imekamilisha makubaliano ya kumsajili golikipa Senne Lammens raia wa Ubeljiji akitokea Royal Antwerp FC, huku akitarajiwa kusaini mkataba wa miaka mitano.
Lammens mwenye umri wa miaka 23 anatarajiwa kusaini mkataba mpya na mashetani hao wekundu wa old trafford kabla ya kufungwa kwa dirisha la usajili leo Septemba 1, 2025.