Baada ya kuwasili Bongo Alfajiri ya leo Clatous Chama jioni ya leo amefanya mazoezi yake ya kwanza na uzi wa klabu ya yake mpya ya Singida black stars.
👉🏽 Kumbuka Chama amejiunga na Singida black stars kama mchezaji huru baada ya kumalizana na Young Africans. Singida Black stars wamempatia mkataba wa mwaka mmoja.
👉🏽 Mazoezini Chama ameonekana amevalia Jezi namba 7 ambayo ni jezi maarufu zaidi kwasababu inavaliwa na moja ya wachezaji bora duniani Cristiano Ronaldo.
👉🏽 Kesho Singida black stars Watacheza na Polisi kenya kwenye mchezo wa Cecafa kagame Cup saa 10:00 jioni.