Mwaka mmoja baada ya kuongoza Bodi ya Wakurugenzi ya Simba SC, bilionea na mwekezaji wa klabu hiyo, Mohammed Dewji (MO), ametangaza kujiondoa katika nafasi hiyo na kumteua Crescentius Magori kuwa Mwenyekiti mpya.
Akitangaza uamuzi huo leo Septemba 4, 2025, Dewji amesema amebanwa na majukumu binafsi na mara nyingi kuwa mbali na shughuli za kila siku za klabu, hivyo akiona ni muhimu nafasi hiyo ichukuliwe na mtu mwenye muda na ukaribu zaidi.
Amesisitiza kuwa ataendelea kubaki Rais na Mwekezaji Mkuu wa Simba SC, huku akiwashukuru wajumbe wa bodi waliotangulia kwa mchango wao mkubwa katika maendeleo ya klabu.
Kwa mujibu wa Katiba ya Simba Sports Club Company Limited, Rais ana mamlaka ya kuteua viongozi wa bodi. Dewji ametumia mamlaka hayo kumteua Magori, sambamba na kuteua wajumbe saba wa bodi upande wake:
Barbara Gonzalez
Hussein Kitta
Azim Dewji
Rashid Shangazi
Swedi Mkwabi
Zuly Chandoo
George Ruhango