TANGA: MSANII maarufu wa Bongo Fleva nchini Tanzania, Rose Ndauka, ametoa shukrani kwa mashabiki na Watanzania wote kufuatia ajali ya gari aliyopata hivi karibuni akiwa njiani kutoka Dar es Salaam kuelekea Tanga.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Rose aliandika ujumbe wa kipekee akitoa shukrani kwa mapenzi makubwa aliyooneshwa na mashabiki, wananchi wa kawaida, pamoja na Jeshi la Polisi.
“Ahsanteni sana wapenzi wangu kwa mapenzi yenu makubwa sana mliyonionesha na mnayoendelea kunionesha… Ahsante,” ameandika.
Alieleza kuwa ajali hiyo ilitokea majira ya saa 11:30 alfajiri, ambapoilivyo bahati hakuna aliyepoteza maisha, ingawa wote waliokuwemo kwenye gari walipata majeraha na kwa sasa wanaendelea na matibabu.
Katika ujumbe huo, Rose pia alitoa taarifa ya kupotea kwa pochi yake nyeusi yenye mistari, ambayo ndani yake kulikuwa na pasipoti, pesa taslimu, na simu aina ya iPhone 16. Alitoa namba ya mawasiliano kwa yeyote atakayeiona:
+255 716 995 561 Rose Ndauka
Aidha, aliwashukuru kwa dhati Watanzania wasiojulikana waliowasaidia mara baada ya ajali hiyo, pamoja na askari polisi wa Michungwani kwa kuwa wa kwanza kufika eneo la tukio na kuwapeleka hospitali.
“Tunapenda kutoa shukrani za dhati kwa Watanzania tusio wafahamu lakini wametusaidia na kuhakikisha tunapata msaada – mbarikiwe sana. Bila kusahau askari polisi wa Michungwani waliotuokoa na kutupeleka hospitalini,” aliongeza.
Rose pia aliwaomba mashabiki wanaotaka kumuunga mkono kifedha kutumia namba hiyo hiyo aliyoweka hadharani.
The post Rose Ndauka atoa shukrani baada ya kupona ajali first appeared on SpotiLEO.