Klabu ya Simba imeutangaza uwanja wa Benjamini Mkapa kuwa uwanja watakaoutumia kama uwanja wao wa nyumbani katika mashindano yote kwa msimu wa mwaka 2025/26.
Simba wamerejea kwenye uwanja huo ambao wamekuwa wakiutumia kama uwanja wa nyumbani kwa misimu mingi kabla ya msimu jana kuahamia KMC Complex ili kupisha marekebisho yaliyokuwa yanafanyika katika uwanja huo.