NEW YORK: TALAKA ya Jennifer Lopez kutoka kwa Ben Affleck ilikuwa “jambo bora zaidi ambalo limewahi kutokea” kwake hiyo ni kwa mujibu wa Mwanamuziki na muigizaji wa filamu mbalimbali Jenifer Lopezi.
Mwimbaji huyo mwenye umri wa miaka 56 alifunga ndoa na muigizaji Ben Affleck mwaka 2022, lakini walitengana mwaka2024 baada ya miaka miwili ya ndoa na Jennifer anasisitiza kuwa talaka ilikuwa nzuri kwake kwa sababu ilimsaidia kujitambua zaidi.
Wakati wa kuonekana kwenye CBS Sunday Morning, Jennifer alifunguka kuhusu kufanya kazi na mume wake wa wakati huo kwenye filamu yake ya Kiss of the Spider Woman – iliyotengenezwa na Affleck kwa kushirikiana na kampuni ya Matt Damon
“Filamu isingetengenezwa, ilikuwa vigumu kutofikiria juu ya mambo lakini ilikuwa, kama, nyakati bora na mbaya zaidi. Kila wakati tulipoketi … nilifurahi sana. Kisha … nyumbani, haikuwa nzuri.”
Hata hivyo, Jennifer ameazimia kuona upande mzuri wa uzoefu huo.
Aliongeza: “Lakini unaimaliza na, unajua, kwa uaminifu, lazima niseme, ilikuwa jambo bora zaidi ambalo limewahi kunipata kwa sababu lilinibadilisha.
“Ilinisaidia kukua kwa njia ambayo nilihitaji kukua … kujitambua zaidi. Mimi ni mtu tofauti sasa kuliko nilivyokuwa mwaka jana.”
Wenzi hao walitengana mnamo Aprili 2024 na talaka yao ilikamilishwa mnamo Januari, na Jennifer aliendelea kukiri kwamba alikuwa na msimu wa joto mzuri na anaweza kupata furaha maishani.
Hapo awali Affleck alifunguka kuhusu mgawanyiko katika mahojiano na jarida la GQ mapema mwaka huu, akisisitiza kuwa hakuna lolote nyuma ya uigizaji wao wa filamu ya Pamoja kwa kuwa ndoa yao ilishavunjika na kila mtu anaishi kwa furaha.
“Ni hadithi tu kuhusu watu wanaojaribu kujua maisha na uhusiano wao kwa njia ambazo sisi sote hufanya kawaida.”
The post Jennifer Lopez: Talaka ilikuwa jambo bora sana kwangu first appeared on SpotiLEO.