WAKATI tetesi zikieleza kuwa mabosi wa Yanga SC huenda wakaachana na Kocha Mkuu, Romain Folz ambaye amekiongoza kikosi hicho kutwaa taji la Ngao ya Jamii, Legend katika masuala ya michezo Tanzania Saleh Ally Jembe amehoji maswali mazito.
Jembe amebainisha kuwa tetesi hizo haoni kama zina mashiko kutokana na sababu ambazo zinatajwa kutoeleweka kwani hakuna kitu ambacho hajakifanya kocha Folz.
“Ikiwa utasema kwamba Yanga SC wanataka kumuacha Folz inabidi unaiambie kwa nini anaachwa kwa sasa? Ukiangalia ameongoza mechi tano na hajafungwa.
“Mchezo wa kirafiki, mchezo wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC ambao ulikuwa na ushindani mkubwa. ukiachana na hilo kuna mchezo wa kimataifa Ligi ya Mabingwa Afrika ameshinda mechi zote mbili.
“Kocha aliyepata ushindi wa jumla ya mabao 5-0 kimataifa unataka umfukuze kwa sababu ipi? Ina maana makocha wote ambao wamepata matokeo tofauti na Folz nao wafukuzwe? Kuna namna ambayo ipo kuhusu uchezeji naona wengi watakuwa hawajui.
“Tangu zamani Yanga SC imekuwa na aina ya mchezo wa kutafuta ushindi yaani ni mpira wa mbio kisha wao wanatafuta matokeo leo hii useme wanacheza vibaya wamfukuze kocha sijui kama itakuwa hivyo lakini tusubiri na tuone,”.
Yanga SC Septemba 30 2025 itakuwa na mchezo wa ligi ya NBC dhidi ya Mbeya City unaotarajiwa kuchezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.