Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026
Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026Msimu wa 2025/2026 wa Ligi Kuu NBC Tanzania umeanza rasmi leo, Septemba 17, ambapo mashabiki wa soka nchini wamefurahia kushuhudia pambano la ufunguzi lililozikutanisha timu za Coastal Union na Tanzania Prisons. Katika mchezo huo uliojaa ushindani, Coastal Union iliibuka kidedea baada ya kuibamiza Tanzania Prisons bao 1–0, ushindi ambao uliwapa mwanzo mzuri katika safari yao ya msimu huu mpya wa ligi.
Msimu huu wa 2025/2026 unatarajiwa kuwa wenye ushindani mkubwa zaidi ukizangatia mabadiliko makubwa ya vikosi na benchi la ufundi yaliyofanywa na vilabu mbalimbali haswa Azam Fc, Singida Bs, Simba Sc na YantgaJe, Yanga SC wataweza kutetea ubingwa wao?
Azam FC, Singida Bs na Simba SC zitaweza kumaliza utawala wa Yanga msimu huu? Je, tutashuhudia timu zingine zikiibuka na kuwa miongoni mwa washindani wakuu? Maswali haya na mengine mengi yatajibiwa kadri msimu huu utakavyokuwa ukiendelea.
Mashabiki wa soka Tanzania wana kila sababu ya kutazamia msimu uliojaa msisimko, ushindani mkali, na mshangao mwingi. Ligi Kuu ya NBC 2025/2026 inaahidi kuwa msimu ambao hautakumbukwa tu kwa matokeo yake, bali pia kwa ubora wa soka litakalochezwa.
Msimamo wa Ligi kuu NBC Tanzania 2025/2026 | Msimamo Ligi Kuu Bara
Pos | Timu | P | W | D | L | GF | GA | GD | Pts |
1 | Singida Black Stars | 2 | 2 | 0 | 0 | 2 | 0 | 2 | 6 |
2 | Young Africans | 2 | 1 | 1 | 0 | 3 | 0 | 3 | 4 |
3 | Dodoma Jiji FC | 3 | 1 | 1 | 1 | 4 | 3 | 1 | 4 |
4 | JKT Tanzania | 2 | 1 | 1 | 0 | 3 | 2 | 1 | 4 |
5 | Namungo FC | 2 | 1 | 1 | 0 | 2 | 1 | 1 | 4 |
6 | Mashujaa FC | 3 | 1 | 1 | 1 | 2 | 2 | 0 | 4 |
7 | Mbeya City | 3 | 1 | 1 | 1 | 1 | 2 | -1 | 4 |
8 | Simba | 1 | 1 | 0 | 0 | 3 | 0 | 3 | 3 |
9 | Azam FC | 1 | 1 | 0 | 0 | 2 | 0 | 2 | 3 |
10 | Mtibwa Sugar | 2 | 1 | 0 | 1 | 2 | 1 | 1 | 3 |
11 | KMC | 3 | 1 | 0 | 2 | 1 | 2 | -1 | 3 |
12 | Tanzania Prisons | 3 | 1 | 0 | 2 | 1 | 2 | -1 | 3 |
13 | Coastal Union | 3 | 1 | 0 | 2 | 2 | 4 | -2 | 3 |
14 | Tabora | 2 | 0 | 2 | 0 | 2 | 2 | 0 | 2 |
15 | Pamba | 3 | 0 | 2 | 1 | 1 | 4 | -3 | 2 |
16 | Fountain Gate | 3 | 0 | 0 | 3 | 0 | 6 | -6 | 0 |
- MP- Michezo Iliyochezwa (Match Played)
- W- Ushindi (Winsi)
- D- Sare (Draw)
- L-Kufungwa (Lose)
- GF- Magoli Ambayo Timu Imefunga (Goal For)
- GA- Magoli Ambayo Timu Imefungwa (Goals Against)
- GD- Tofauti Ya Magoli (Goal Difference)
- PTS- Jumla Ya Alama (Points)