Simba vs Namungo FC Leo 01/10/2025 Saa Ngapi?
Wekundu wa Msimbazi Simba leo watakua dimbani kuzisaka pointi tatu muhimu za Ligi Kuu ya NBC Tanzania Bara 2025/2026 mbele ya wageni wao Namungo FC katika mchezo unaotajwa kuwa wa ushindani mkubwa. Mchezo huu utapigwa katika Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam kuanzia saa 2:15 usiku, ukitarajiwa kuvuta hisia za mashabiki kutokana na historia na rekodi za timu hizi mbili.
Simba vs Namungo FC Leo Saa Ngapi?
Mchezo kati ya Simba SC dhidi ya Namungo FC utafanyika Leo, Jumatano tarehe 01 Oktoba 2025, kuanzia saa 2:15 usiku, kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa jijini Dar es Salaam.