INAELEZWA kuwa Bulgaria Dimitar Pantev mwenye miaka 49 huenda akapewa mikoba ya kukinoa kikosi cha Simba SC ambacho kwa sasa hakina kocha mkuu.
Taarifa zinaeleza kuwa muafaka mzuri umefikiwa kwa pande zote mbili ambapo mpango kazi ukikamilika atakuja Tanzania kuchukua nafasi ya Fadlu Davids aliyepata dili Raja Casablanca na tayari ameanza kazi.
Inaelezwa kuwa Simba wamekubali kulipa fidia za kuvunja mkataba wa kocha huyo aliyekuwa anaifundisha Klabu ya Gaborone United ya Botswana.
Ikumbukwe kwamba Gaborone United ilicheza na Simba SC katika Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali, katika mchezo uliochezwa Dar kocha huyo alikuwa kwenye benchi la ufundi la Gaborone United.
Kocha huyo aliwahi kuzifundishwa klabu za Orapa United, Victoria United na FC Johansen anatarajiwa kuwasili nchini Tanzania mwishoni mwa wiki kukamilisha mpango kazi wa kujiunga na Simba SC.