WAKATI tetesi zikieleza kuwa huenda Romain Folz akafutwa kazi ndani ya kikosi cha Yanga SC rekodi zinaonyesha kuwa amekiongoza kikosi kwenye mechi 6.
Katika mechi hizo ushini ni mechi tano na aliambua sare mchezo mmoja wa ligi ugenini dhidi ya Mbeya City uliochezwa Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Sababu kubwa inayotajwa kumuondoa Folz kwenye benchi la ufundi ni timu kucheza katika kiwango cha chini katika mechi za ushindani.
Hizi hapa rekodi za mechi ambazo alikaa benchi ndani ya msimu wa 2025/26 mrithi wa mikoba ya Miloud Hamdi:-
Yanga 1-0 Bandari ya Kenya. (Mechi ya kirafiki)
Yanga SC 1-0 Simba SC, (Ngao ya Jamii).
Wiliete 0-3 Yanga SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).
Yanga SC 3-0 Pamba Jiji, (Ligi ya NBC).
Yanga 2-0 Wiliete SC, (Ligi ya Mabingwa Afrika).
Mbeya City 0-0 Yanga SC, (Ligi ya NBC)