DAR ES SALAAM:MSEMAJI wa klabu ya Simba, Ahmed Ally, ameonya mashabiki wanaoingia kwenye mkumbo wa kumzungumzia Kocha vibaya na kutaka kuamini kuwa Dimitar Pantev ana uwezo mkubwa wa kurejesha heshima yao.
Mapema wiki hii klabu hiyo, ilimtambulisha Kocha huyo kuchukua nafasi ya Fadlu Devids aliyetimkia Morocco. Lakini alitambulishwa kama Meneja Mkuu.
“Achaneni na maneno ya wapagazi mara sijui kocha kafanyeje, kocha tuliyemleta ana uwezo wa kutuvusha na kufika mbali. Lengo la kumleta ni kurejesha heshima ya Simba, kurejesha mataji yaliyopotea na hiyo kazi anaiweza kwa asilimia kubwa.
Alisema wana imani naye na matumaini makubwa atainua timu na kurejesha heshima ya klabu hiyo.
Katika hatua nyingine, Wekundu hao wa Msimbazi kwa kushirikiana na watengenezaji wa jezi zao wamekuwa na kampeni kwenye mikoa mbalimbali ili kutoa elimu kwa mashabiki namna ya kutambua jezi halali na feki.
“Kuna njia nyingi za kubaini jezi ni halali au sio halali. Ukinunua uka-scani kitu fulani kinakupeleka kwenye tovuti. Jezi feki hazina ubora,” alisema Msemaji huyo.
Simba inahamasisha mashabiki kuendelea kununua jezi za asili kupitia maduka rasmi na magari ya usambazaji yaliyoratibiwa na klabu ili kulinda sifa ya timu na hali ya ushindani ambayo inahitaji msaada wa wapenzi wote.
The post Ahmed: Dimitar Pantev atarejesha heshima yetu first appeared on SpotiLEO.