Ibenge: Hakuna Mechi Rahisi CAF – Azam FC Lazima Iwe Makini Dhidi ya KMKM
Kocha mkuu wa Azam FC Florent Ibenge amewaonya wachezaji wake kutarajia mchezo mgumu wanapokutana na KMKM katika michuano ya CAF. Ibenge alisisitiza kuwa katika hatua hii ya mashindano hakuna timu dhaifu, kwani kila timu inayofika hapa inaonyesha ubora na maandalizi ya hali ya juu.
👉 “Nimewaambia wachezaji wangu kwamba hakuna mchezo rahisi katika mashindano ya CAF. Timu yoyote inayofika hatua hii ina ubora. Tusipokuwa makini tutajikuta tunapata matokeo yasiyotabirika,” alisema Ibenge.
Kocha huyo raia wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) amekuwa akijulikana kwa nidhamu na mbinu bora za kiufundi, na sasa analenga kuhakikisha Wanalambalamba wanaendelea na mwenendo mzuri katika michuano ya kimataifa.
Ibenge amesema maandalizi ya kikosi chake yamekuwa mazuri, lakini akasisitiza umuhimu wa umakini, nidhamu na kutumia nafasi wanazopata uwanjani, akiamini kwamba michezo ya CAF mara nyingi huamuliwa na makosa madogo.
Azam FC, ambao wameonyesha maendeleo makubwa katika soka la Tanzania na Afrika Mashariki, wanatarajiwa kutumia uzoefu wa wachezaji wao wa kimataifa kuhakikisha wanapata matokeo chanya dhidi ya KMKM,
Mashabiki wa soka wanatarajia pambano hilo kuwa la ushindani mkubwa, hasa ikizingatiwa kuwa timu zote mbili zinatoka kwenye ukanda mmoja, jambo linaloongeza ladha ya “derby ya Kisiwa cha Unguja na Bara.”