Mwanachama hai wa klabu ya Yanga Sc anayejulikana kwa majina ya Mzee Magoma ameibuka na taarifa nzito juu ya hatma ya klabu hiyo kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu huu.
Mzee Magoma katika taatifa yake aliyoitoa siku ya leo Jumanne tarehe 21 Oktoba ameeleza wazi kwamba Rais wa klabu ya Yanga Sc wa sasa Eng. Hersi Said ndiye kirusi kinachoitafuna klabu hiyo kwa sasa licha ya kwamba mashabiki hawaelewi kuhusiana na jambo hilo.
Mzee Magoma katika taarifa yake ameendelea kueleza kwamba Rais Hersi Said kwa sasa anajiona kama yeye ndio yeye na kwamba anaifanya klabu ya Yanga Sc kama yakwake peke yake kitu ambacho hakifai katika namna ya kuiongoza klabu hiyo.
Mzee Magoma ametanabaisha kwamba Rais Hersi Said anatakiwa kujua kwamba Yanga Sc ina watu wake na watu wenyewe ndio wanachama kama yeye (Mzee Magoma) na wanachama wengine ambao wamekuwa sehemu ya timu hiyo kwa miaka mingi sana.
Mzee Magoma katika taarifa yake amefika mbali zaidi kwa kueleza kwamba kama wanachama wa Yanga Sc watafanya maamuzi ya kumuachia Hersi Said mechi ijayo ya marudioni ambayo Yanga Sc watacheza dhidi ya Silver Strikers Oktoba 25 kwa Mkapa, Yanga Sc hawawezi kutoboa kwa maana kwamba hawatafika katika hatua ya makundi ya ligi ya mabingwa barani Afrika msimu huu.
Mzee Magoma amemtaka Hersi Said apunguze kujiona mkubwa sana ndani ya klabu ya Yanga Sc badala yake atengeneze mfumbo ambao utakua ni mfumo shirikishi baina ya viongozi wa klabu ya Yanga Sc pamoja na mashabiki pamoja na wanachama wa klabu hiyo ili kutengeza umoja ndani ya timu yako.