Anaitwa:
Pedro Valdemar Soares Gonçalves bealizaliwa tarehe 7 Februari 1976 mjini Lisboa, Ureno. Ni kocha wa soka mwenye uzoefu mkubwa, aliyewahi kufanya kazi katika klabu mbalimbali za Ureno kama Amora FC na Sporting CP, ambako alisaidia kukuza wachezaji wengi chipukizi.
Mwaka 2015 alihamia Angola na kufanya kazi na klabu ya Primeiro de Agosto kabla ya kuteuliwa kuwa kocha wa timu ya taifa ya vijana U-17. Chini ya uongozi wake, timu hiyo ilifanikiwa kufuzu kwa mara ya kwanza katika historia ya Angola kushiriki Kombe la Dunia la U-17, jambo lililoimarisha jina lake katika soka la Afrika.
Mwaka 2019, Gonçalves aliteuliwa kuwa kocha mkuu wa timu ya taifa ya Angola (Palancas Negras). Ameiwezesha timu hiyo kucheza soka la kisasa na kupata mafanikio makubwa, ikiwemo ushindi wa kihistoria dhidi ya Ghana. Amejulikana kwa nidhamu, ubunifu, na uwezo wa kukuza wachezaji wenye vipaji barani Afrika.







