Imani ni kwake Baba aliye juu Mbinguni, Prince.
Kuna nyakati Mwanadamu unaweka sana jitihada kwenye Maisha, unavuja jasho lako lote, unatumia nguvu zako na uwezo wako wa kila aina, lakini mwisho wa siku haupati matokeo unayoyatamani.
Inatokea hii Prince. Inaweza kumtokea Mkulima shambani, inaweza kumtokea Mama sokoni na inaweza kumtokea Ronaldo kwenye uwanja wa mpira.
Inamtokea Yoyote. Kipindi kipindi unachopitia sasa hivi Prince uwanjani kinaweza kumtokea mwanadamu yoyote anayevuta pumzi ya Mungu Duniani.
Walio salama ni wale tu walio lala futi 6 chini ya Tumbo la ardhi. Lakini kama bado uko hai, unapumua, Tegemea jaribu la Mungu wakati wowote.
Na sio kwamba hufanya hivyo kwa kuwa anatuchukia, hapana. Jaribu lolote lile, kubwa au dogo huja kwa ajili ya kutukumbusha kuwa, tuko Sisi Tunaotamani na Yuko yeye Muumba, anayepanga.
Matamanio yetu ya mambo/vitu vizuri yanahitaji mpango wake.
Ukikosa leo, unatakiwa usiku urudi tena kwenye sala, kumuomba akupangie kesho nzuri.
Tunapaswa Kumuomba na Kumtegemea Mungu Pekee.
Wanaofeli Duniani sio wale wanaokosa Bali ni wale wanaopoteza imani. Najua Imani yako ni Imara sana @mgadafiprince.73 👊🏼🙏🏼
Jumbe zote za Mashabiki wa @yangasc ni za kukumbusha kuwa, wewe ni sehemu ya Familia yetu. Tulishawahi kwenye hali kama hii ya leo huko nyuma, Na tukasimama na wewe pamoja.
Wananchi wanakuahidi kusimama na wewe Tena, kwa sala na Maombi na In Shaa Allah. Furaha itarudi tena kwenye uso wako na kwenye mioyo yao tukiruka na kushangilia Mabao yao uwanjani.
Wanayanga wanaona jitihada zao. Wanaona unavyokimbia zaidi uwanjani kuipambania Timu ishinde, kinachokosena ni Magoli tu kutoka mguuni mwako.
Tuna imani kubwa Yatapatikana. Tunaomba na wewe Uamini pia. Tuko pamoja.
Tuweke kichwa juu Prince na Jumanne In Shaa Allah, Mashabiki wa @yangasc Watakuja tena KMC kukushangilia kwa sauti ya juu ukiwa kwenye Jezi yao👊🏼🏟️







