DAR ES SALAAM: MWIMBAJI wa Nyimbo za Injili nchini, Obby Alpha, amesema kuwa hata mtu akiwa na utajiri na mali nyingi, bado dunia inaweza kuonekana chungu endapo ataishi peke yake bila kuwa na watu wengine.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Obby Alpha ameandika ujumbe unaohimiza umuhimu wa watu katika maisha ya kila siku, akieleza kuwa thamani ya vitu tulivyonavyo hutegemea uwepo wa wengine.
“Mfano sisi sote tuondoke duniani tukuache na kila kitu kilichopo leo… sidhani kama utaona umuhimu wa chochote pasipokuwa na huyo jirani yako. Hii ina maana kwamba dunia haitakuwa na ladha yoyote kama asingekuwepo huyo jirani yako,” ameandika.
Ameongeza kuwa baadhi ya watu wanaposhiba au kupata mafanikio, husahau kwamba nao ni binadamu kama wale ambao hawajapata mafanikio, jambo linalopelekea kukosekana kwa utu na upendo.
“Pasipo watu, utu, upendo amani na ushirikiano… dunia si tamu. Maana watu ndiyo chumvi ya ulimwengu,” amesema akirejea maandiko ya Mathayo 5:13.
The post “Dunia bila watu haina radha” – Obby Alpha first appeared on SpotiLEO.






