DAR ES SALAAM: BONDIA Ramadhan Mkwakwate maarufu kama Sungu Mtata anatarajiwa kupanda ulingoni kuvaana na mpiganaji mwenye nguvu kutoka DR Congo, Regan Pacho, katika pambano la kimataifa litakalopigwa Desemba 26, 2025 Dar es Salaam.
Akizungumza wakati wa maandalizi yake Chamanzi, Mkwakwate alisema amejiandaa kikamilifu kuhakikisha ushindi unabaki nyumbani.
“Maandalizi ni asilimia mia. Mashabiki waje kuona kazi, ushindi lazima,” amesema Ramadhan Mkwakwate
Mashabiki na wadau wake kutoka Chamanzi wameonesha imani kuwa Pacho hatakuwa tishio, wakisisitiza kuwa siku hiyo haitakuwa ya muziki bali vita ya masumbwi.
“Wakongo wajulikane kwa muziki, lakini siyo Desemba 26. Ushindi unabaki hapa,”Salum Hatibu, Shabiki
“Tumejipanga kuhakikisha Mkwakwate anaibuka na ushindi,” Sebastian Deo, Mdau
Kocha wake, Jafari Baruti, alisema mpiganaji wake yuko kwenye ubora mkubwa na yuko tayari kwa mapambano.
Katika usiku huo wa Boxing on Boxing Day, mabondia mbalimbali watapanda ulingoni akiwemo nyota wa ngumi Hassan Mwakinyo atakayongoza mpambano huo maalum.
The post Mkwakwate kuvutana na Mcongo Desemba 26 first appeared on SpotiLEO.


