WAKATI wanachama wa Simba wakisomewa ripoti ya mapato na matumizi, wameonyesha kukoshwa na rais wao wa heshima Mohammed Dewji ‘MO’ na namna anavyoipa fedha klabu hiyo.
Mhasibu wa Simba Suleiman Kahumbu wakati akisoma ripoti ya mapato ya msimu uliopita amesema MO Dewji alichangia kiasi ha sh 4 Bilioni kwenye bajeti yao ya mwaka ujao wa fedha.
Mara baada ya Kahumbu kusema hivyo wanachama wa Simba wakiishangilia kwa nguvu huku wakipigia makofi taarifa hiyo.
Aidha Kahumbu akaendelea akisema katika bajeti ya msimu huu 2025-26, MO amechangia kiasi cha Sh 6 Bilioni kwenye bajeti yao.
Kahumbu akaongeza, fedha hizo za MO tayari zimeshaingizwa katika akaunti ya Simba ambazo ndio zimefanya usajili wa wachezaji wao msimu huu.
Baada ya kutangazwa hivyo wanachama hao tena wakashangilia kwa nguvu huku wakisimama na kuanza kuimba jina la Bilionea hiyo wakisema MO MO MO MO.
Kwa takwimu hizo, Mo Dewji anakuwa amechangia zaidi ya Bil 10 kwa msimu wa 2025/26- 26/27 , hii imekuwa ni nnje ya zile Bil 20 alizotoa kwa ajili ya uwekezaji ambao hata hivyo bado haujaanza kufanya kazi kulingana na baadhi ya taratibu kutokukamilika.
The post MO DEWJI BABA LAO SIMBA…..ATOA BIL 10 ZA USAJILI MSIMU 25/26-26/27…..MASHABIKI ROHO KWATUU… appeared first on Soka La Bongo.



