DAR ES SALAAM: MFANYABIASHARA Jennifer Jovin maarufu kama Niffer ametoa shukrani za dhati kwa watu waliomfariji na kumtembelea kipindi alipokuwa gerezani, akiwemo Paula Paul, Marioo na mama yake Kajala Masanja.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Niffer aliandika ujumbe mrefu akionyesha namna alivyoguswa na upendo na ukaribu aliopata kutoka kwa familia hiyo.
“Thank you! Ulikuwa wa kwanza kuungana na rafiki zangu kuja gerezani kuniona weekend ya kwanza kabisa! Na ukaniachia mpunga wa kutosha! Na mara ya pili tena ukaja na familia nzima! Wewe, Kajalafrida, mariootz… I was more than happy!! Allah awalipe kheri sana!
“Asanteni sana kwa moyo wenu wa upendo. Mungu awabariki sana. Nawapenda leo na kesho. Allah aepushe hasad na macho ya uovu baina yetu! Nyie ni Familia. Asanteni kwa kumpa faraja mama yangu! She is so grateful to you kwa kila hali.” ameandika Niffer.
Amesema kitendo cha Paula na Kajala kumtembelea na kumfariji kimeacha alama kubwa kwake na kwa familia yake, hasa mama yake ambaye aliguswa na upendo huo.
The post Niffer awashukuru Mastaa waliotembelea Mahabusu first appeared on SpotiLEO.





