DAR ES SALAAM:MSANII wa filamu na muziki wa Bongo Fleva, Irene Uwoya, ameomba msamaha kwa Mungu baada ya kukiri kukosea katika mawazo, maneno na matendo yake.
Kupitia ukurasa wake wa Instagram, muigizaji huyo maarufu nchini Tanzania alichapisha ujumbe wenye kuonesha unyenyekevu na majuto makubwa akisema:
“Mungu naomba unisamehe (GOD please forgive me)… nimekosa sana kwa mawazo, maneno, matendo… please GOD moyo wangu mzito sana… bila wewe mimi ni bure… nimeenda kinyume na mapenzi yako… please forgive me
,” aliandika Irene Uwoya.
Ujumbe huo umeibua hisia mbalimbali miongoni mwa mashabiki na watumiaji wa mitandao ya kijamii, wengi wakimpongeza kwa ujasiri wa kujitathmini na kuchukua hatua ya kutubu hadharani.
Hatua hiyo ya Irene Uwoya imeonekana kama ishara ya unyenyekevu na dhamira ya kuanza upya maisha yake kwa kumrudia Mungu, jambo linaloendelea kupata uungwaji mkono mkubwa kutoka kwa wadau wa sanaa na jamii kwa ujumla.
The post Irene Uwoya atangaza kutubu na kuanza maisha mapya first appeared on SpotiLEO.









