Akina mama wajawazito na waliojifungua hivi karibuni katika Hospitali ya Palestina, Sinza jijini Dar es Salaam, wamepata faraja ya kipekee mwishoni mwa mwaka huu baada ya kupokea msaada wa Mama Packs kutoka Meridianbet. Msaada huo umejumuisha mahitaji muhimu ya mama na mtoto kama nguo za watoto wachanga, nepi, wipes, sabuni pamoja na taulo za kike, ukiwa na lengo la kusaidia kipindi cha awali cha malezi.
Msaada huo umetolewa kama sehemu ya utekelezaji wa Uwajibikaji wa Kampuni kwa Jamii (CSR) wa Meridianbet, unaolenga kushiriki kikamilifu katika kuboresha maisha ya jamii. Kampuni hiyo imekuwa ikitambua umuhimu wa kuwekeza katika ustawi wa jamii inayoiwezesha kufanya shughuli zake za kila siku, hususan kwa makundi yenye uhitaji maalum.
Akizungumza wakati wa tukio hilo, Afisa Mawasiliano wa Meridianbet alisema kuwa kampuni inaamini kuwa mafanikio ya biashara yanapaswa kuwa na mchango chanya kwa jamii. Alieleza kuwa msaada huo wa mwisho wa mwaka umetolewa ili kuwapa akina mama matumaini mapya, faraja na nguvu ya kuanza mwaka mpya wakiwa na tabasamu.
Meridianbet haikuachi nyuma, kuna michezo mbalimbali ya kasino mtandaoni pamoja na mechi za kimataifa za kubashiri zenye odds bomba zinazokuongezea nafasi ya kuongeza kipato chako kila siku. Kujiunga ni rahisi! Tembelea meridianbet.co.tz au piga *149*10#.
Kwa upande wa Hospitali ya Palestina, uongozi wake ulipokea msaada huo kwa shukrani kubwa, ukieleza kuwa umefika wakati muafaka. Mwakilishi wa hospitali hiyo alisema kuwa msaada huo utapunguza baadhi ya changamoto wanazokutana nazo akina mama wakati wa kujifungua na baada ya kujifungua, huku akipongeza Meridianbet kwa moyo wake wa kujali.
Kwa ujumla, hatua hiyo inaendelea kuithibitisha Meridianbet kama mdau anayejali maendeleo ya jamii. Kupitia miradi mbalimbali ya kijamii katika sekta za afya, elimu na michezo, kampuni hiyo imeendelea kujenga uhusiano imara na jamii, ikionesha kuwa mafanikio ya kibiashara yanaweza kwenda sambamba na kugusa maisha ya watu kwa njia chanya na endelevu.
The post MERIDIANBET KUIBUA FARAJA WAMAMA PALESTINA appeared first on Soka La Bongo.




