PEMBA: MSHAMBULIAJI mpya wa Yanga SC, Allan Okello, hakuna kuchelewa tayari ameanza mazoezi Leo ( jana ) na wenzake mara baada ya kuwasili na kujiunga rasmi na klabu hiyo.
Okello anaonekana mwenye hamasa kubwa na ari ya kufanya mazoezi Gym akionesha kuwa yupo tayari kwa changamoto mpya ndani ya Ligi Kuu ya NBC.
Mchezaji huyo amesajiliwa kutoka klabu ya Vipers SC ya Uganda, akiwa na uzoefu mkubwa wa soka la Afrika Mashariki na mashindano ya kimataifa.

Ujio wake unaongeza ushindani mkubwa katika safu ya ushambuliaji ya Wananchi, huku benchi la ufundi likitarajia kunufaika na kasi, ufundi pamoja na uwezo wake wa kufumania nyavu.
Okello, ambaye pia ni mchezaji wa timu ya taifa ya Uganda (The Cranes), anatajwa kuwa mmoja wa wachezaji mahiri waliowahi kung’ara kwenye Ligi Kuu ya Uganda na mashindano ya klabu barani Afrika.
Mashabiki wa Yanga wanatarajia kumuona akitoa mchango mkubwa katika harakati za kutetea ubingwa wa ligi na kufanya vizuri kwenye michuano ya kimataifa msimu huu.
The post Okello hakuna kuchelewa ameanza kazi rasmi first appeared on SpotiLEO.






