Kamishina Msaidizi wa Idara ya Uendelezaj wa Sekta ya Fedha, Bi. Dionesia Mjema, akitoa mada kuhusu masuala ya fedha na umuhimu wa kusajili vikundi vya kutoa huduma ndogo za fedha na vile vya kijamii kwa wananchi wa Kata ya Makanya, kwenye program maalum ya elimu ya fedha iliyotolewa kwa wananchi hao katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Makanya Wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.
Afisa Usimamizi wa Fedha katika Idara ya Uendelezaji wa Sekta ya Fedha – Wizara ya Fedha, Bw. Stanley Kibakaya akifafanua kuhusu masuala ya mikopo salama na umuhimu wa kusajili vikundi vya kutoa huduma ndogo za fedha kwa wananchi na wanafunzi wa Kata ya Makanya kwenye program maalum ya elimu ya fedha iliyotolewa katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Makanya wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.
Afisa Ushirika, Tume ya Maendeleo ya Ushirika, Bw. Adolf Felix Ndunguru, akitoa mada kuhusu masuala ya fedha na umuhimu wa kusajili vikundi vya kutoa huduma ndogo za fedha kwa wananchi na wanafunzi wa Kata ya Makanya kwenye program maalum ya elimu ya fedha iliyotolewa katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Makanya wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.
Afisa Mkuu kutoka Benki Kuu ya Tanzania, (BoT), Mwile kauzeni akitoa mada kuhusu masuala ya fedha na umuhimu wa kusajili vikundi vya kutoa huduma ndogo za fedha kwa wananchi na wanafunzi wa Kata ya Makanya kwenye program maalum ya elimu ya fedha iliyotolewa katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Makanya wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.
Mratibu wa huduma ndogo za fedha same DC, Bw. Ally Msumi, akitoa mada kuhusu masuala ya fedha na umuhimu wa kusajili vikundi vya kutoa huduma ndogo za fedha kwa wananchi na wanafunzi wa Kata ya Makanya kwenye program maalum ya elimu ya fedha iliyotolewa katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Makanya wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.
Afisa wa Uendeshaji wa Mfuko Wa Uwekezaji Wa Pamoja Wa Wekeza Maisha (UTT AMIS) Tawi la Arusha, Bw. Elias Nyakimura Muhoji akitoa mada kuhusu masuala ya fedha na umuhimu wa kusajili vikundi vya kutoa huduma ndogo za fedha kwa wananchi na wanafunzi wa Kata ya Makanya kwenye program maalum ya elimu ya fedha iliyotolewa katika ukumbi wa Shule ya Sekondari Makanya wilaya ya Same Mkoani Kilimanjaro.

Baadhi ya wajasiriamali na wananchi pamoja na wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Makanya, Wilayani Same mkoani Kilimanjaro, wakipata elimu ya fedha kwa njia ya filamu yenye maudhui kuhusu matumizi sahihi ya fedha, umuhimu wa kupanga bajeti na kuitekeleza, umuhimu wa kusajili vikundi vya huduma ndogo za fedha , utunzaji wa fedha binafsi, umuhimu wa kushirikisha familia na watu wa karibu kwenye masuala ya fedha na uwekezaji, umuhimu wa kukata bima ya biashara na mali nyingine, filamu hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha lengo likiwa ni kusambaza elimu ya fedha kwa njia rahisi ya burudani ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa masuala ya huduma za fedha.
Baadhi ya wajasiriamali na wananchi pamoja na wanafunzi kutoka Shule ya Sekondari Makanya, Kata ya Makanya, Wilayani Same mkoani Kilimanjaro, wakichangia mada mbalimbali kuhusu elimu ya fedha waliyoipata kupitia njia ya filamu yenye maudhui kuhusu matumizi sahihi ya fedha, umuhimu wa kupanga bajeti na kuitekeleza, umuhimu wa kusajili vikundi vya huduma ndogo za fedha , utunzaji wa fedha binafsi, umuhimu wa kushirikisha familia na watu wa karibu kwenye masuala ya fedha na uwekezaji, umuhimu wa kukata bima ya biashara na mali nyingine, filamu hiyo imeandaliwa na Wizara ya Fedha lengo likiwa ni kusambaza elimu ya fedha kwa njia rahisi ya burudani ili kuhakikisha wananchi wanapata uelewa wa masuala ya huduma za fedha.
…………………